WENGI WAJITOKEZA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA KILIMO BIASHARA CHA PAPAI SALAMA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange
(kulia), akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu
Edger Mwamfupe katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya
Spice leo makutano ya Mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Dar es Salaam
leo.Taasisi hizo zitashirikiana katika nyanja za teknolojia na Kilimo
kwa lengo la kuunganisha nguvu za umoja ili kuwapunguzia wananchi
umasikini.
ZAIDI
ya wanachama 500 wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita),
wanatarajiwa kushiriki mafunzo maalum ya kufungua msimu wa kilimo cha
Papai salama.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkikita, Adam Ngamange wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Ngamange
alisema mafunzo hayo yatafanyika Februari 24 mwaka huu yatabeba ujumbe
'Papai salama open speech' kwa lengo la kuunganisha walaji, wazalishaji
na wataalam wa kilimo hicho.
Alisema
baada ya tafiti kufanyika wamegundua mkanganyiko mkubwa wa taarifa
hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi mabadiliko katika kilimo cha Papai
yatatokea."Tafiti
zinaonesha watalaam wanatofautiana kwenye idadi ya miche, uchimbaji wa
mashimo, umwagiliaji maji na utiaji mbolea hivyo mafunzo haya yataweka
washiriki kwenye mstari ili kukidhi ubora na ulinganifu wa soko la ndani
na nje," alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema mafunzo hayo yatawakutanisha wabobezi na watendaji
mbalimbali katika kilimo hicho kipya cha Papai salama yatakuwa na awamu
tatu tofauti ili kujenga misingi imara katika kuleta unafuu wa
uzalishaji papai.Alisema
Mkikita imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wakulima wa Tanzania
hasa wanaolima papai, mchaichai, mhogo na pilipili kichaa.
Aidha,
Ngamange alisema pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kupokea ugeni
kutoka nchini Uturuki kutambua fursa za zao la papai nchini.Pia
alisema wanachama wa Mkikita wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo
Nchini Israel kuanzia Machi 11 mwaka huu na kugharimu dola za Marekani
2,000.
Halikadhalika
Mkikita imesaini makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Hope For All
ambayo ina wanachama zaidi ya 5,000 ili waweze kushirikiana kwenye
nyanja za teknolojia na kilimo.Akizungumzia
makubaliano hayo Mkurugenzi wa Hope For All Edgar Mwamfupe alisema
matarajio yao ni kuona mkulima anaheshima katika jamii.
Mwamfupe alisema kupitia Mkikita wanachama wao watafikia kwenye umilionea kwa kuwa kuna fursa za soko na biashara.
Ngamange
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya
semina ya mafunzo ya Kilimo biashara cha Papai Salama.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger
Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari na kuelezea ni kwa
nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi
masikini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger
Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari na kuelezea ni kwa
nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi
masikini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui
na Adam Ngamange.
Mratibu
wa Ziara ya Utalii Kilimo Israel, Bw. Kizito (kulia), akielezea umhimu
wa ziara hiyo pamoja na faidha watakazozipata watakaokwenda.
Mfanyabishara
Adamjee (kulia) akielezea kuhusu kilimo cha pilipili kichaa na faida
zake. Adamjee amekubali kujiunga na Mkikita ili kusaidiana kutafuta
masoko ya zao hilo ndani na nje ya nchi.
Ngamange akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akielezea kazi mbalimbali za mtandao huo
Askofu Mwamfupe na Adam Ngamange wakitliana saini makubaliano ya ushirikiano
Mtaalamu wa Kilimo cha Zao la Pilipili Kichaa, akielezea faida ya zao hilo pamoja na matumizi mbalimbali ya pilipili
Ofisa
Uhusiano wa Mkikita, Neema akielezea taratibu za wanachama na wasio
wanachama jinsi ya kushiriki kwenye semina ya Kilimo cha Kisasa cha
Papai Salama.
Mmiliki
wa Spice Hotel Ltd, Mwangaba (kulia) akizungumza na uongozi a Mkikita
uliokutana naye baada ya kufanya mkutano na wanahabari kwenye hoteli
hiyo ya Kisasa.
Post a Comment