TANZANIA; WAKULIMA WAMEANZA KULIMA MIHOGO KAMA ZAO LA BIASHARA KUTOKANA NA UHITAJI MKUBWA



Ni jioni. Lakini Joram Mikanda  bado yupo shambani, Akitazama kama mihogo imekomaa tayari kwa kuuzwa. Mr Mikanda nimkulima mzoefu wa mihogo, amekua akilima mihogo tango mwaka 1990, na ametumia jitihada zake zote katika kulima mihogo.

  Mr. Mikanda anaishi katika kijiji cha Kitahana kilichopo mkoani kigoma, ambapo kunamahitaji makubwa ya mihongo kwaajili ya kutengeneza bia na kusafirisha katika nchi jirani. 

  Kimila, watu wa ukanda huu wa Tanzania hawali sana mihogo, hupenda kutumia maindi kwaajili ya kutengeneza uga wa kupika ugali. Lakini kulingana na uhitaji wakulima wengi wameamaska kulima mihogo. kama zao la biashara. Wakulima husafirisha mihogo kwenda Burundi, Rwanda na Congo.

Mr. Mikanda anaelezea; nauza mihogo mibichi katika soko la ndani na pia na safirisha mihogo mikavu nje ya nchi.... Kwanzia 1990 nimeku nikisafirisha mihogo kwenda burundi kwa kutumia baisikeri na nimekua nikiuza shilingi 20 hadi 50 kwa kilo  [US$0.01 to US$0.02]  lakini ilikua ningumu na hatari kusafirishamihogo kwa baiskeli nakupita mistuni.

Mr. Mikanda anasema NGOs na maafisa ugani wanahamasisha wakulima kulima mihogo kwa sababu inaitajika sana katika makambi ya wakimbizi na pia katika nchi jirani. 

 Christopher Chubwa ni mkulima katika kijiji cha Kitahana alie anza kulima mihogo kama zao la biashara mwaka 2000, na sasa anaweza kusaidia familia yake kwa kupitia mapato ya mihogo na anauza mihogo katika kambi la wakimbizi la Nduta na pia anasafirisha mihogo mibichi na mikavu katika nchi za Rwanda, Burundi, Congo, naUganda.” 

Mr. Chubwa anasema kwake shamba la mihogo nikama mgodo, anasema watu pia wameanza kutengeneza unga wa mihogo kwaajili ya wanyama na binadamu.Anaongezea kusema wameunda kikundi cha wakulima 25 na wanataka kujenga jengo kwaajili ya kuprocess mihogo.

Victor Kabunga ni afisa ugani na amefanya kazi kwa miaka tisa katika wilaya ya kibondo inayohusisha kijiji cha kitahama, mara kwa mara huwatembelea wakulima wa mihogo kufahamu jinsi wanavoendelea.na kuwapa ushauri. Anasema anawaelimisha wakulima wa mihogo , kama vile umbali wa kupanda na jinsi ya kuchagua miche bora, anaongeza kua wakulima na wafanya biashara wanapata kibari cha kuuza nje ya nchi kupitia wizara ya kilimo., anasema mwanga sasa unaonekana kwa wakulima wa mihogo na ndoto zake ni kuuza mihogo Africa nzima na ndio maana wanampango kwa kuanzisha kiwanda cha kuprocess mihogo.
 Anasema wanaiomba serikali kuboresha miundombini katika mkoawa kigoma ili kuwawezesha kusafirisha bidhaa zao bila usumbufu. Pia anasema mihogo imebadili maisha yao , anaelezea musimu ulio pita alitumia kipato alichopata kulipa ada za wanae.

kazi hii imetengenezwa na AGRA, the Alliance for a Green Revolution in Africa, kama sehemu ya mradi na kutafsiliwa na IMANI LUBABA.

No comments