WAKULIMA WA MAHARAGE WANAWEZA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAHARAGE KWA KUBADILI MBINU ZA UVUNAJI NA USAFIRISHAJI
Ni msimu wa mavuno kanda ya kaskazini magharibi mwa Tanzania. Monica
Lugesha akiwa amvaa vazi buluu ya kung’aa na waridi na kitambaa. Mama
huyu wa miaka 70 anaonekana akiwa akivuna maharage, anafurahia matunda
ya kazi yake.
Bi. Lugesha anaishi wiliya ya Ngara kata ya Rulenge. Anasema,
wakulima wengi wanapoteza maharage yao wakati wanapovuna shambani na
wanaposafirisha maharage.
Bi. Lugesha anajaribu kupunguza upotevu wa maharage wakati wa kuvuna
na kusafirisha. Anasema, “Nina vuna maharage yangu na kuyasafirisha
nyumbani kwangu. Hapo nyumbani nina anika maharage yangu katika
turubai.”
Anasema wakulima wengi wanavuna maharage kwa kung’oa shina zima na
kufunga mashina hayo kwa kamba na nisha kusafirisha kwa kubeba kichwani
kupeleka nyumbani. Anaelezea: “Chochote tunachokivuna tunakipoteza
kwasababu vibebea vya maharage vinapasuka na mbegu kudondoka shambani.
Wakulima wengine wanasafirisha maharage kwa kutumia pikipiki au
baisikeli, na maharage mengi yanadondoka njiani.”
Mastidia Venus pia ni mkulima wa maharage wilayani Ngara. Mkulima
huyu wa miaka 40 anasema wakulima wanaweza kupoteza mpaka kilo 10 za
maharage katika shamba la hekari moja wakati wa kuvuna na kusafirisha.
Adronizi Bulindoli ni mkulima mwingine wa maharage wilayani Ngara.
Anasema wakulima wengi wilayanai wanavuna maharage shambani wakti yakiwa
yamekauka sana, ambapo inasababisha vibebea/vifuko vya maharage
kupasuka na kudondosha mbegu shambani.
Bw. Bulindoli anasema ni vigumu sana kuokota mbegu za maharage
shambani zinapodondoka, anawashauri wakulima wengine wavune maharage
wakati wa asubuhi amabapo jua sio kali sana.
Essau Nyamziga ni afisa ugani wa eneo hili. Anakubaliana na Bw.
Bulindoli kwamba kuvuna maharage pindi yanapokuwa yamekauka sana
inapelekea kupoteza mbegu za maharage na hivyo kupata hasara.
Anawahimiza wakulima kuvuna maharage pindi yanapobadili rangi na kuwa ya
kijivu na kutumia mifuka kusafirisha na kuhifadhi maharage.
Constatine Mdende ni afisa kilimo umwagiliaji wa wiliya ya Ngara.
Anakadiri kuwa kiasi cha tani 46,000 za maharage zitavunwa mwaka huu
katika wilaya yake, na kati ya tani hizi, tani 2,300 zitapotea. Anasema
wakulima wabebe maharage katika mifuka imara ya plastiki kuepuka
kudondoka kwa mbegu za maharage wakati wa kuvuna na kusafirisha.
Mbali na kumtegemea maafisa ugani kutoka wiliayani kuwapatia elimu,
wakulima wanapaswa kupata elimu kutoka vyanzo mbadala kama vipindi vya
kilimo redioni. Frank Ademba ni afisa miradi wa shirika la Farm Radio
International, sjirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi hapa
wiliyani na Redio Kwizera kuzalisha vipindi vya kilimo redioni. Anasema
vipindi vya redio vinawashawishi wakulima kulima maharage, ikigusia mada
za upandaji, mavuno, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na
masoko.
Mkulima mmoja wapo aliye weza kusikiliza vipindi na kubadili namna ya
uzalishaji, uvunaji na uhifadhi wa maharage ni Sophia Metusera kutoka
kijiji cha Kumuzuza wilaya ya Ngara. Akiwa anatembea katika shamba lake
akibeba mbegu zilizo vunwa za maharage katika mifuko yeye na wenzake,
anasema, “Nina pendelea kusafirisha mbegu za maharage kuliko kusafirisha
[mmea mzima wa maharage], kwasababu kubeba mmea mzima wa maharage
vibebea vinaweza kupasuka na kudondosha mbegu za maharage.”
Bi. Metusera anasema anasema alijifunza namna ya kuzalisha maharage
kupitia vipindi vya Redio Kwizera. Anaongeza, “Nataka kuwa mkulima bora
kijijini kwangu.”
Post a Comment