KILIMO NI MOJA YA SEKTA INAYO WEZA KUAJIRI VIJANA WENGI.


Vijana wa Jifunze wakitoa elimu kwa vitendo Pwani ( picha na mpiga picha wetu)

Kama tunavyo fahamu kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu, na ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda nilazima sekta ya kilimo itiliwe mkazo. Kwamaana hiyo, sekta ya kilimo ni moja ya sekta ambayo inaweza kuchangia asilimia kubwa katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini. Kwa kutambua hilo baadhi ya vijana wameanza kutambu fursa na kuzichangamki hivyo wamefanikiwa kupiga hatua katika maisha yao ya kila siku kama tulivo fanya mahojiano na mmoja wa vijana hao.

Jifunze kilimo  
Obison Obadia ni kijana alie jikita katika kilimo, ufugaji, ujasiriamali na uhamasishaji. Anasema kikubwa nafanya kilimo na ufugaji napia ninawahamasisha wengine kuingia kwenye biashara ya kilimo pia ni muanzilishi wa Jifunze kilimo.
Anasema, Jifunze kilimo ni taasisi binafsi iliyosajiliwa kwa lengo la kuhamasisha watu hasa vijana kujiingiza katika kilimo biashara kama njia ya kujiajili na kuajili vijana wengine kwaajili ya kujiletea maendeleo. Anasema..  Hasahasa tunatoa elimu kwa mazao ambayo sisi tunalima kama matikiti, matango, hoho, bamia, nyanya chungu, mahindi, mihogo, viazi lishe na mbogamboga za majani zote( cahinizi, mnavu, tembele, maboga na spinachi).
Jifunze kilimo imeanzishwa rasmi mwaka jana. Na nipo peke yangu ingawa kwenye shughuli za uelimishaji na ufundishaji kilimo huwa nashirikiana na wenzangu  @elimu_biashara na @kilimo_smart na kwasasa bado nipo mkoa wa pwani maeneo ya mlandizi, rufiji na kisarawe, pia nipo kigamboni na mwakani natarajia kwenda kuwekeza zaidi Morogoro na Tanga.
Obadia anasema.., anapitia changamoto nyingi sana kubwa zikiwa ni mtaji na masoko hasa ya nje., Anasema mwaka 2018 nilipanga kulima heka zaidi ya 100 za mahindi ila sikufanyikiwa, kwanza niliitaji kua na eneo langu mwenyewe ambalo ningefunga miundombinu yote ya kisasa, niliitaji kua na mashine yangu ya kufanya packaging. Ilishindikana kwakua sikua na mtaji huo pamoja na jitihada nyingi za kutafuta hata mikopo kwenye benki ya wakulima TADB.Anaendelea Nilipata bahati ya kupata masoko ya Nje ya Nchi kusafirisha baadhhi ya matunda ila mlolongo wa kufanikisha zoezi zima niliishia katikati na dili nikalikosa.

Malengo yako ni nini?
 Vijana wakiwa kazini
Anasema malengo yangu ni kua mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo hii itaenda sambamba na kuzalisha ajira nyingi, kua msambazajimkubwa wa pembejeo za kilimo, kusaidia wakulima katika kupata masoko na pia kua taasisi kubwa ya kutoa elimu ya ujasiriamali hasa katika Nyanjaya kilimo. Anaendelea.., Nimejipanga sana katika kutatua changamoto ninazopata. Nashukuru nimeshaanza kupata wadau wakubwa wa kushirikiana nao katika baadhi ya miradi.
Kuhusu masoko  pia nimeshaanza kupata connection ya baadhi ya wabunge na mawaziri ambo wanaweza wakanisaidia katika kutatua hizo changamoto hasa kupata miongozo  kwenye taasisi za serikali.

Nini kifanyike  ili kilimo kiwe na tija?
Kwa mujibu wa Obadia anashauri serikali na wadau wa kilimo; sekta ya kilimo ni moja ya sekta kubwa inayoweza kuajiri vijana wengi kwa wakati mmoja na kupelekea kuondokana na tatizo la ajira nchini. Nini kifanyike?
“Serikali, Taasisi za kilimo ziweke mazingira rafiki hasa kwa vijana ili ziweze kuwahamasisha zaidi kuingia kwenye kilimo. Mfano serikali inaweza ikatenga maeneo maalumu ya kilimo kila mkoa, zikawekwa kambi kwa vijana kwenda kulima, wakapewa mikopo rahisi, wakapewa wataalamu wa kuwashauri na kuwasimamia, Baada ya mavuno, kupitia wizara ya viwanda, wizara ya a\mambo ya nje wakashirikiana kutafuta masokoya nje ya hayo mazao. Hii itawahamasisha zaidi watu kuingia kwenye kilimo maana watakua wana uhakika na masoko kwenye mazao wanayolima” Anasema
Pia anatoa lai kwa jamii wasidanganyike na story na calculation za mitandaoni, kwamba ukiweka hela kiasi flani shambani baada ya muda mfupi utapata faida . Hiyo si kweli,
“Kilimo ni biashara kama biashara nyingine yoyote kuna faida na hasara. Tena kilimo kinaweza kikawa na changamoto nyingi zaidi kikubwa inahitaji mtu kujitoa sana na kua mvumilivu. Then ndo utaona matunda yake” anamaliza..

Makala hii Fupi, imeandaliwa Na kuandikwa Na IMANI LUBABA, Na inaletwa kwenu Na mtandao ulio jikita katika kutoa elimu ya kilimo Na ufugaji TANZANIA NA KILIMO kupitia mpango wake wa VIJANA NA KILIMO.
 +255764148221

No comments