Kuloirel ni kuku chotara ambaye asili yake ni nchini india, na imetokana na mchanganyiko wa dume la broiler na jike aina ya Rhode island red au dume la white legham na jike la Rhode island red.
Kuku hawa ni moja kati ya kuku wasio na gharama kubwa katika kuwafuga lakini pia wana faida kubwa pindi ukiamua kuwafuga. Lakini hii ni moja Kati ya aina zinazo fanya vizuri katika nchi nyingi.
Tazama video chini kujifunza zaidi 👇 na usipite bila kusubscribe channel yetu ili uwe karibu nasi zaidi.
Tazama video chini kujifunza zaidi 👇 na usipite bila kusubscribe channel yetu ili uwe karibu nasi zaidi.
SIFA ZA KUROILER
1. Ni aina ya kuku ambao hutumika kwa matumizi ya ani nyama pamoja na mayai.
2. Kuroiler ni kuku anae fugika katika mifumo yote
3. Pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi (disease resistance)
4. Kuku hawa hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu wanauwezo pia wa kula chakula kama kuku wa kienyeji.
BANDA
Kama walivyo kuku wengine banda lazima liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi, ila pia kuku wa aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza sehemu ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakulatofauti na kuku wa kisasa.
Lakini pia ni vyema kila wakati ukazingatia usafi ni muhimu hivyo ni vyema kuzingatia hilo.
CHAKULA
Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
1. Muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya chakula mwenyewe.
2. Kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha kuanzia (chick starter mash)
3. Kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick grower mash)
4. Kuanzia wiki ya kwanza kuanza kutaga hadi mwisho unatakiwa kuwapa chakula(layersm ash)
5. Katika ufugaji wa kuku hawa ni muhimu kuzingatia lishe bora tangu kifaranga hadi kuanza kutaga, fahamu kwamba matunzo ya kuku anae anandaliwa kwa ajili ya kuja kuwa mtagaji ni tofauti na yule kuku anae fugwa kwa ajili ya nyama. Hivyo kitu moja wapo cha kuzingatia ni lishe bora unaweza nunua dukani au unaweza changanya mwenyewe tu chakula cha kuku wako kwa kutumia formula Nzuri ba Bora.
Kama ulipitwa na video zetu bofya picha hapa chini na subscribe channel yetu 👇
Kama ulipitwa na video zetu bofya picha hapa chini na subscribe channel yetu 👇
Kwa ushauri, biashara, matangazo na mambo mengi usisite kuwasiliana nasi
+255764148221
rubabaimani@gmail.com
+255764148221
rubabaimani@gmail.com
0 Comments