JIFUNZE UFUGAJI WA MENDE

KUTAZAMA VIDEO YA MAFUNZO HAYA BOFYA HAPA

UTANGULIZI

Ufugaji wa mende ni ufugaji unaokua kwa kasi sana hapa nchini, hii ni kutokana na faida zinazoaminika kupatikana kwa mende.Hivyo kwa namna hii kasi ya ufugaji inaongezeka, kunauwezekano mkubwa sana kwa wafugaji wengi kuingia katika ufugaji huo ha hivyo kuongezeka kwa ushindani.Ufugaji wa mende hauna masharti mengi sana na pia hua na gharama ndogo katika kufuga licha ya kuaminika  kua na  faida.

Kuna Aina zaidi ya 400 za mende duniani na katika hizo aina 30 pekee ndio zinapatikana katika makazi ya watu, lakini  katika hizo aina 4 ndio ambazo ni sumbufu majumbani. Ila mende ambao wamefanyiwa utafiti kwaajiri ya chakula cha kuku, binadamu na hata kutengeneza dawa za urembo ni mende wa Asia ambao wamechanganywa katika aina 3 ili kuweza kupata aina moja bora zaidi (breeding) na aina hizi ni mende wa Asia, Ujerumani na Marekani na kwa kitaalamu mende huyu huitwa diloptera punctuate.

 


MATUMIZI/FAIDA ZA MENDE

Ø Faida ya kwanza mende hutumiwa kama chakula na hata hapa Tanzania kuna watu wanakula mende licha ya soko kubwa kwaajili ya chakula huaminika kua nchini Denmark, brazil na china

Ø Mende pia ni chakula kizuri sana kwakuku na imedhibitishwa kua na kiasi kingi cha protein ukilinganisha na vyakula au wadudu wengine hivyo wafugaji hupendelea kutumia mende kwenye mchanganyo wa chakula kuliko dagaa.

Ø Lakini pia  kwa upande wa taaluma, practical nyingi kwa watu walio pata bahati ya kusoma masomo ya biologia, hutumia mende hivyo unaweza kupata fursa katika upande huu wa taaluma. Kwani mende kwaajili ya practical inaweza kua changamoto kwa mashule.

 

UTAGAJI

Kwa kawaida Mende huchukua muda wa miezi miwili na nusu kufikia wakati wa kuvunwa endapo atapatiwa chakula, maji kwa wakati huchukua hadi miezi minne na hua na uwezo wa kuishi hadi miaka minne kuanzia kuzaliwa hadi kufa. Mende hawa wa kisasa ndio mende wanaotaga mayai mengi zaidi kuliko aina zingine duniani, na mende mmoja hua na uwezo wa kutaga kuanzia mayai 55 hadi 70 na hutaga mara 3 kwa mwaka, na hua tayari kufikia umri wa kuvunwa kwa muda wa miezi miwili na nusu, kwa kawaida endapo watapatiwa mazingira rafiki asilimia kubwa ya mayai hua na uwezo wa kuhenguliwa.

 

JINSI YA KUTENGENEZA BANDA

Banda la kufugia mende linaweza kujengwa kwa mtindo tofati tofauti, hii ni kulingana na eneo mtaji na idadi unayotaka kufuga. Hii ni kutokana na sababu kwamba endapo utataka kufuga mende kwaajiri ya chakula kwa binadamu nilazima uweke mazingira mazuri na rafiki zaidi kuliko mtu anaetaka kufuga kwaajiri ya chakula cha mifugo na endapo mtu anataka kufuga kwa wingi zaidi basi nilazima mabanda nayo yawe mengi na makubwa.

Zamani jamii iikua inamchukulia mende kama mdudu mchafu asie na faida, lakini sasa watu wanajenga mabanda makubwa kwaajili ya kufuga mende majumbani kwao.Hivyo zingatia hivi wakati unafikili kujenga banda la mende.

Ø Andaa eneo maalumu kwaajili ya kufugia

Ø Kumtafuta fundi kwaajili yaujenzi wa banda

Ø Kama nataka kujenga banda kubwa kwaajili yauzarishaji mkubwa unaweza kujenga chmba chanye futi 11 kwa 12

Ø Lakini hakikisha chumba havivuji na hakuna dirisha kubwa kwaani mende hawapende mwanga kabisa. Lakini unaweza kuweka taa ndani ya chuba ili ikusaidia wakati wa kutoa huduma.

NOTE;kujenga chumba ni kwaajiri ya wazarishaji wanaotaka  kufuga kwa wingi na kwa ukubwa na nitatoa maelekezo kidigo kwa wazarishaji wadogo.

Wao hutakiwa kuteua chumba maalumu kwajiri ya kufugia na kuweka mazingira mazuri namaana kutengeneza mazingira ya giza ndani ya chumba, na kudhibiti watu kuingia ndani ya chumba hicho kwani mende huogopa sana mwanga na watu. Na ndani ya chumba unaweza kutengeneza meza maalumu ambazo ndizo zitatumika  kuweka masanduku ya kufugia mende.

 Kuna masanduku maalumu yaliyo tengenezwa kwaajili ya kufugia mende, lakini unaweza kutengeneza sanduku lako mwenyewe kwakutumia mbao, lakini zingatia kutengeneza kwa namna amBayo haiwezi kuruhusu mende kutoka nje au mwanga kuingia ndani ya sanduku.

Zingatia kutengeneza sanduku ambazo zina ukubwa wa kuruhusu trey za mayai kuingia ndani kwaani ni muhimu kuweka trey za mayai zile za karatasi ndani ya sanduku. Kwaan ndio sehemu ambayo mende watatumia kutaga na kujificha.

Kwa wazarishaji wakubwa baada ya kujenga chumba unatakiwa utengeneze frem kama za duka katika kuta za chumba chote na kisha unatengeneza kila frem iwe na mlango ambao haita ruhusu mende kutoka nje.

KUTAZAMA VIDEO YA MAFUNZO HAYA BOFYA HAPA

CHAKULA

Kwa upande wa chakula mende ni kama ilivyo kwa mifugo mengine kua chakula ni muhimu sana kwa ukuaji, mfano kuku uhitaji chakula cha kutosha na chenye mchanganyo sahihi kumuwezesha kukua na kutaga vizuri.

Lakini katika ufugaji wa mende imekua tofauti kidogo kwaani chakula cha mende hakina  formula ambazo unatakiwa kuzingatia wala haigharimu kwa  kiasi kikubwa katika kuwalisha na kuwahudumia, Kwa sababu mende hula aina tofauti tofauti ya chakula  na ambazo zinapatika kirahisi bila gharama kubwa.

Ø Mende hula unga wa  mahindi na unga wa muhogo

Ø Viazi mviringo vilivyo vizima na vile ambavyo vimeharibika

Ø Matunda ya aina mbalimbali

Ø Maharage yaliyopikwa unaweza kuyapondaponda

Ø Mbogamboga

NOTE; Endapo utawapa chakula cha kutosha kila baada ya wiki mbili utakua unavuna kwani watakua washafikisha uzito wa gram 5 ambayo ndio uzito unaofaa zaidi.

SOKO

Kwa upande wa soko kiukweli tunapo elekea hadi sasa hali inazidikua nzuri, kwani watu wengi wameshakua na uelewa na ufugaji huu na hivyo masoko yamezidi kuongezeka ikiambatana na muongezeko wa wafugaji wengi wa mende. Soko la mende limegawanyika katika  sehemu hizi.

Chakula kwa binadamu na wateja wakubwa wanaaminika kua ni wachina hasa kwa hapa Tanzania, lakini pia wengine husafIrIsha nje ya nchi hivyo endapo utaanza kuona watu wanakufahamu pia soko uongezeka.

Kwa upande wa chakula cha mifugo kwa sasa wafugaji wengi wa kuku wamekua wakitumia mende kama mbadala ya dagaa hivyo kwa upande huu soko hukua kwa kasi sana.

Lakini pia kwa upande wa taaluma unaweza kuorganize na mashule mbalimbali na ukawa unawapelekea mende kwaajili ya matumizi ya kitaaluma.

Lakini pia soko lingine ni kwa wafugaji wapya yaani muitikio wawafugaji kuanza kufuga umeongezeka, na licha ya kua na uhaba mkubwa sana wa kupata mbegu, hivyo hii ni fursa kwa wafugaji ambao tayari wameanza kufuga.

 KUTAZAMA VIDEO YA MAFUNZO HAYA BOFYA HAPA

Imani Lubaba,

Email: rubabaimani@gmail.com

Phone: +255764148221

Website: https://tanzanianakilimo.blogspot.com

Youtube: https://youtube.com/rubabaimani

 

No comments