Tunafahamu kwamba chakula kikubwa cha ng’ombe ni nyasi, lakini nyasi pekee haziwezi kumfanya ng’ombe wa maziwa aweze kutoa maziwa ya kutosha na yaliyo bora. Kwa sababu nyasi pekee hazitoshi kumpa virutubisho vyote muhimu. Hivyo kwa mfugaji anaetaka kupata matokeo mazuri nilazima azingatia kuwapa lishe bora ng’ombe wake.Ili waweze kutoa maziwa mengi na yenye ubora, ngombe wa maziwa wanaitaji lishe bora. Na ili lishe iwe bora ni lazima iwe na mchanganyiko wa virutubisho vyote kwa uwiano sahihi ambavyo ni:-
Nguvu
Protini
Vitamin
Madini
Maji
NGUVU
Tunafahamu kwamba majani ndio chakula kikuu cha ngombe, unapompa mlisha majani ngĂłmbe wako mpe mchanganyiko wa majani makavu nusu na majani mabichi nusu.
Malisho mabichi yapo ya aina nyingi sana ambayo unaweza kutumia Lucerna, majani ya viazi vitamu au majani ambayo tunayatumiakila siku katika kuwalisha ngombe na majani yakiwa mabichi ndani yake hua na kiasi cha maji kingi.
Zingatia kutokumlisha ngĂłmbe majani ambayo yametoka kukatwa muda huo, kata majani mabichi na uyaweke katika chumba chenye giza kisha katakata vipande vya inchi 2 au 5 cm ili kumlaishishia ngĂłmbe wakati wa kula na itasaidiaupotevu wa majani. Hivyo unaweza kuweka utaratibu mzuri wa kukata nyasi na kuzitunza kama ilivyo elekezwa hapo juu
Ngombe wa maziwa anatakiwa kupewa kilo 15-20 za majani mabichi kwa siku, na inapendeza sana ukawapa kwa awamu mbili mfano asubuhi na jioni.
Malisho makavu nayo yapo ya aina nyingi sana mfano mabua ya ngano na mahindi na hata majani ya kawaida yakiwa makavu.
Wakati wakuwalisha changanya sehemu moja ya malisho makavu na sehemu moja ya malisho mabich, yaani kwa uwiano sawa mfano gunia moja ya nyasi za napier na gunia moja ya mabua ya mahindi yaliyo katwa katwa.
MAJI
Kumbuka kua maji ni malighafi muhimu sana katika utengenezaji wa maziwa mwilini kwa ng’ombe, hivyo kuwapa maji safi na mengi kila siku ni muhimu sana.Toa maji kwenye chombo cha majikila baada ya siku 3 na weka maji safi, hii itasaidia sana katika kuzuia magonjwa.
JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA ZIADA NYUMBANI
Kwa ng’ombe anae kula nyasi pekee ni ngumu sana kutoa maziwa mengi hata kama ng’ombe ni bora pia, hivyo ni muhimu sana kuwapa chakula cha ziada. Lakii=ni changamoto inakuja kwa wafugaji upande wa kununua chakula cha ziada kwani vinaweza kua na gharama kubwa hivyo kuwafanya wafugaji wasipate faida Hivyo ili kuepuka yote hayo tunashauri utengeneze chakula hicho nyumbani mwenyewe. Na endapo ukitengeneza nyumbani ni vyema sana kwa sababu hua nafaidia zifuatazo.
Ni rahisi sana
Upunguza gharama ukilinganisha na kununua dukani
Hua na ubora kwani utahakikisha unatumia marighafi bora.
Ili chakula kiweze kua na manufaa nilazima kitengenezwe kwa uwiano sahihi wa nguvu, proteini na madini
Mfano wa vyakula vinavyotoa nguvu
Mapumba ya mpunga
Ngano isiyo kobolewa
Sukari guru
Mapumba ya mahindi
Mfano wa vyakula vinavyotoa protein
Majani ya lucerne
Mashudu ya pamba
Soya
Mashudu ya alizeti
Majani ya msesibania
Majani ya calliandra
Dagaa walio sagwa
Vyanzo vya madini
Hupatina katika maduka ya mifugo
Dicalcium Phosphorate
Jiwe la chumvi
Phosposphate ya miamba
Mchanganyiko wa mdini(mineral mix)
Jinsi ya kuchanganya kwa uwiano sahihi
A. Chakula cha ziada cha awali hiki anapewa ng’ombe wa maziwa ambae hakamuliwi. Mchanganyo wa kilo mia unatakiwa kuchanganya kwa uwiano huu.
Kilo 75 za chakula kinacho toa nguvu
Kilo 23 chakula cha protein
Kilo 2 ya madani.
KUFAHAMU ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA
0764148221
rubabaimani@gmail.com
KUTAZAMA VIDEO YA MAFUNZO HAYA BOFYA PICHA CHINI
0 Comments