Moja ya furaha yetu kubwa kama Jukwaa la Kilimo na Ufugaji ni kushiriki ujuzi na maarifa tuliyonayo ili jamii yetu ifaidike. Ndiyo maana tumevutiwa sana kufanya kazi na Koudijs, kampuni inayoongoza katika sekta ya lishe bora kwa mifugo. Koudijs haileti tu bidhaa bora sokoni, bali pia inatoa elimu ya lishe na ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji ili kuongeza tija katika shughuli zao za ufugaji.
Hivi karibuni, tulitembelea eneo la Katoro, Geita tukiwa pamoja na Dr. Emmanuel, mwakilishi wa Koudijs kanda ya Ziwa, kwa lengo la kuhakikisha wafugaji wa kuku wa mayai wanapata elimu ya bure kuhusu lishe sahihi ya mifugo yao. Katika kikao hiki, tulizungumzia umuhimu wa kutumia vyakula vyenye virutubisho kamili ili kuongeza uzalishaji wa mayai na kuboresha afya ya kuku.
Kama mfugaji, unapotumia lishe sahihi, unapata faida nyingi, zikiwemo:
Kuongezeka kwa uzalishaji wa mayai – Kuku wanaolishwa kwa chakula chenye virutubisho kamili hutoa mayai kwa wingi na yenye ubora wa hali ya juu.
Kupunguza gharama za matibabu – Lishe bora huimarisha kinga ya mwili ya kuku, hivyo kuwapunguzia magonjwa.
Kuongeza faida – Unapopunguza gharama za matibabu na kuongeza uzalishaji wa mayai, faida katika ufugaji wako inaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Katika mkutano wetu Katoro, tulileta Concentrates bora za Koudijs ambazo ni suluhisho sahihi kwa wafugaji wanaotaka kuongeza uzalishaji wao. Concentrates hizi zimeundwa kitaalamu ili kutoa virutubisho vyote muhimu kwa kuku wa mayai, kusaidia ukuaji wao na kuongeza uzalishaji wa mayai kwa muda mfupi.
Ikiwa uko Kanda ya Ziwa na unahitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu lishe ya mifugo au unataka kupata bidhaa bora kwa bei rafiki, tupo tayari kukufikia!
📞 Wasiliana naO sasa kupitia 0765321406 ili tuweze kukusaidia kuboresha ufugaji wako!
0 Comments