WAZO LA KIBIASHARA: WEKEZA 280,000 KWA MWEZI KATIKA NG’OMBE WA MAZIWA, UPATE HADI 930,000!


Hivi karibuni tulitoa andiko kwamba ukifuga ng'ombe wa maziwa mmoja tu, unaweza kupata kati ya TSh 600,000 hadi 900,000 kwa mwezi. Pia, tulieleza jinsi hii ilivyo fursa kubwa kwa watu wengi, hasa wale wanaoishi mijini.

Leo hii nakuletea mchanganuo wa gharama, mapato na faida, ili uone mwenyewe jinsi unavyoweza kuanza na kufanikiwa katika ufugaji huu.

Gharama za Uendeshaji kwa Mwezi

Katika maeneo ya mijini kama Dar es Salaam, gharama za kumhudumia ng'ombe mmoja wa maziwa kwa mwezi zinajumuisha:

  • Chakula (nyasi na virutubisho kama pumba, mashudu, na mifugo feeds) – TSh 150,000 - 300,000

  • Matibabu na Chanjo – TSh 10,000 - 20,000

  • Maji – TSh 20,000 - 50,000

  • Ulinzi na Wafanyakazi (ikiwa unamwajiri mtu) – TSh 100,000 - 200,000

  • Gharama nyingine (banda, umeme, vifaa) – TSh 10,000+

Jumla ya Gharama kwa Mwezi: TSh 280,000 - 570,000 


Makadirio ya Mapato kwa Mwezi

Ng'ombe wa maziwa mwenye ubora mzuri anaweza kutoa wastani wa lita 15 - 25 kwa siku.

Kwa bei ya maziwa ya TSh 1,700 - 2,000 kwa lita, unaweza kupata mapato yafuatayo:

  • 15 lita x 30 siku x 1,700 = TSh 765,000 kwa mwezi

  • 25 lita x 30 siku x 2,000 = TSh 1,500,000 kwa mwezi

Jumla ya Mapato kwa Mwezi: TSh 765,000 - 1,500,000


Makadirio ya Faida kwa Mwezi

Faida = Mapato - Gharama

  • Faida Ndogo (gharama kubwa, uzalishaji mdogo):
    TSh 765,000 - 280,000 = TSh 485,000

  • Faida Kubwa (gharama ndogo, uzalishaji mkubwa):
    TSh 1,500,000 - 570,000 = TSh 930,000

Kwa ng’ombe mmoja tu wa maziwa, unaweza kutengeneza faida ya TSh 485,000 hadi 930,000 kwa mwezi!

Faida Nyingine za Ufugaji wa Ng’ombe wa Maziwa

  • Kusindika maziwa – Badala ya kuuza maziwa ghafi, unaweza kuzalisha bidhaa kama mtindi, siagi na jibini, ambazo huuzwa kwa bei ya juu.

  • Mbolea ya samadi – Samadi kutoka kwa ng’ombe wako inaweza kuuzwa kwa wakulima kama mbolea bora.

  • Ndama wa kuuza – Ng’ombe wako ataendelea kuzaa ndama, ambao unaweza kuuza au kuongeza idadi ya mifugo wako.

Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ni biashara yenye faida kubwa na inayotoa kipato endelevu kila siku. Ukiwa na mipango mizuri na maarifa sahihi, unaweza kukuza biashara yako kwa muda mfupi!


BADO HUJAJIUNGA NA GROUP LETU LA MAFUNZO?

Jiunge leo upate elimu ya kina kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na mbinu za kuongeza

 faida yako! WAILIANA NASI 0764148221

Post a Comment

0 Comments