KOUDIJS Yaendelea Kuwanoa Wafugaji Wa Kuku wa Mayai Kanda ya Ziwa - BURE KABISA !?

0

 

Moja ya malengo makuu ya kampuni ya Koudijs ni kuhakikisha wafugaji wa kuku wanapata siyo tu bidhaa bora zitakazoongeza tija katika shughuli zao, bali pia elimu ya lishe itakayowasaidia kupunguza gharama za uzalishaji, kuboresha afya ya mifugo na kuongeza ufanisi katika ufugaji wao. Kupitia huduma hii, wafugaji wanapewa maarifa sahihi kuhusu lishe bora, usimamizi wa mashamba ya kuku, pamoja na mbinu za kisasa za kudhibiti changamoto zinazojitokeza katika uzalishaji.

Katika kutekeleza dhamira hiyo, Koudijs imeendelea kuwafikia wafugaji moja kwa moja mashambani katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa, ikitoa ushauri wa kitaalamu na elimu ya lishe bure kabisa.

Ziara Kanyama, Kisesa – Mwanza

Mtaalamu kutoka kampuni ya Koudijs hivi karibuni alimtembelea mfugaji wa kuku wa mayai anayepatikana katika eneo la Kanyama, Kisesa Jijini Mwanza. Mfugaji huyu anamiliki mashamba mawili ya kuku wa mayai na ni mmoja wa wafugaji wanaojituma na kuwekeza kwa bidii katika sekta hii.

Licha ya mafanikio aliyoyapata katika shughuli zake za ufugaji, amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa zikiwemo:

  • Kupungua kwa kiwango cha utagaji

  • Kuku kula chakula kingi bila matokeo mazuri

  • Magonjwa yanayotokana na lishe isiyo sahihi

Changamoto hizi zilimlazimu kutafuta msaada wa kitaalamu ili kuboresha uzalishaji na kupunguza hasara.

Koudijs Yatoa Msaada Bila Gharama

Koudijs, kupitia timu yake ya wataalamu, ilichukua jukumu la kumsaidia mfugaji huyu kwa kumtembelea shambani kwake, kufanya tathmini ya changamoto alizokuwa anakutana nazo, na kumpatia elimu ya kina kuhusu lishe sahihi kwa kuku wa mayai.

Aidha, mfugaji huyo alipatiwa pia ushauri juu ya matumizi ya bidhaa bora za kampuni ya Koudijs, hasa aina ya concentrates zinazosaidia kuku kuongeza kiwango cha utagaji, kuboresha afya na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya chakula.

Huduma hii haitolewi kwa mfugaji huyo pekee, bali kwa mfugaji yeyote anayeendesha ufugaji wa kuku wa mayai na anakumbana na changamoto kama hizo, popote ndani ya Kanda ya Ziwa. Koudijs inatoa huduma hii bila malipo yoyote, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuboresha maisha ya wafugaji na kuongeza uzalishaji wa ndani wa mazao ya mifugo.

BOFYA PICHA CHINI KUTAZAMA VIDEO NZIMA

Wasiliana Nasi

Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa mayai na unahitaji msaada wa kitaalamu kuhusu lishe bora au unakumbana na changamoto zinazofanana, usisite kuwasiliana na timu ya Koudijs. Tutakufikia popote ulipo ndani ya Kanda ya Ziwa.

Mawasiliano:

0765 321 406 / 0783 127 406

Koudijs – Lishe sahihi, matokeo bora.
Endelea kufuatilia blog yetu na mitandao ya Rubaba Media kwa taarifa na elimu zaidi kuhusu kilimo na ufugaji nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

write your comment here

write your comment here

Post a Comment (0)

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top