Cage za Kienyeji: Suluhisho la Gharama Nafuu kwa Kila Mfugaji wa Kuku

0

Katika mazingira ambayo wengi huamini kuwa "ufugaji wa kisasa ni kwa matajiri," Mzee Hashimu – afisa mstaafu kutoka Mwanza – anathibitisha kinyume chake. Akiwa na uzoefu wa maisha na ujasiri wa kujaribu vitu vipya, leo anafuga kuku wa Sasso kwa kutumia cage alizozibuni mwenyewe kwa mbao – ndani ya banda lake dogo.

Hakununua kutoka China. Hakusubiri ufadhili. Alitumia kilichopo, kwa maarifa sahihi.

🎯 Cage hizi ni za mbao, lakini zimeundwa kwa akili:

  • Kila moja ina sehemu ya maji yenye nippers, zinazoendeshwa na tanki kubwa moja tu.

  • Gutter ya chakula imetengenezwa kwa ustadi – hakuna upotevu.

  • Sehemu ya kinyesi imepangiliwa kuhakikisha usafi wa ndani ya banda.

Cha ajabu zaidi? Hahitaji eneo kubwa. Banda lake lina nafasi ndogo – lakini uzalishaji ni mkubwa. Ndiyo maana tunasema:
🔑 “Ufugaji si ukubwa wa eneo, ni ukubwa wa maarifa.”

Ungependa kujifunza zaidi mbinu kama hizi?

Kwenye jumuiya yetu ya mafunzo ya Rubaba, tunakutanisha wafugaji wabunifu kama Mzee Hashimu na wengine kutoka kila kona ya nchi. Hapa tunabadilishana maarifa, tunashauriana, na tunakua pamoja.

📲 Jiunge nasi kwa mwaka mzima kwa ada ndogo ya mafunzo:
👉 Bonyeza hapa kuwasiliana nasi WhatsApp

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

write your comment here

write your comment here

Post a Comment (0)

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top