Wakulima wengi wa mpunga hapa Tanzania huvuna gunia chache sana kwa ekari – na kwa bahati mbaya, wengi huamini kuwa hilo ni jambo la kawaida. Lakini je, unajua kuna wakulima wanaovuna hadi gunia 40 kwa ekari moja?
Ndiyo! Wakati wewe unavuna gunia 5 au 7, mkulima mwenzako anakusanya gunia 35 hadi 40 kutoka kwenye ekari hiyo hiyo.
Sasa swali ni moja: Tofauti iko wapi?
Tofauti haiko kwenye hali ya hewa, haiko kwenye udongo tu, bali iko kwenye maarifa na mbinu za kilimo. Kuna aina tatu kuu za mbinu ambazo wakulima hutumia, na kila moja huleta matokeo tofauti kabisa:
1. Kilimo cha Mazoea
Hiki ni kile kilimo cha “baba yangu naye alikuwa analima hivi.” Hakuna kupima udongo, hakuna kutumia mbegu bora wala mbolea ya uhakika. Wakulima wa aina hii huvuna gunia 5 hadi 10 tu kwa ekari — na mara nyingi huingia hasara.
2. Kilimo Bora kwa Ushauri
Hapa mkulima anatumia mbegu bora, anafuata ushauri wa wataalamu, na hutumia mbolea kulingana na ushauri wa msingi (japo si lazima awe amepima udongo). Hapa mkulima anaweza kupata gunia 15 hadi 25 kwa ekari. Si pabaya — lakini bado kuna nafasi ya kuboresha zaidi.
3. Kilimo cha Kisasa
Hii ni ngazi ya juu zaidi. Mkulima anapima udongo kabla ya kupanda, anachagua aina sahihi ya mbegu kulingana na udongo wake, anatumia mbolea na virutubisho kulingana na mahitaji halisi ya udongo, na pia hutumia mfumo wa umwagiliaji au udhibiti mzuri wa maji. Huyu anaweza kuvuna hadi gunia 30, 35 au hata 40 kwa ekari moja.
Chaguo ni lako sasa mkulima:
Je, utabaki kwenye kundi la kilimo cha mazoea kinachokuletea gunia 5, au utapanda ngazi hadi kilimo bora au cha kisasa?
Kumbuka: Mpunga hauhitaji nguvu sana, bali unahitaji maarifa sahihi.
📢 Jifunze Zaidi – Lima Kibiashara!
Usiruhusu miaka iendelee kupotea bila tija. Jiunge nasi leo kwenye jumuiya ya wakulima wa kisasa. Tunakupa maarifa, mbinu, na ushauri wa kitaalamu kila wiki.
🟢 Bonyeza hapa kujiunga WhatsApp na Jumuiya Yetu:
👉 https://wa.me/255764148221
write your comment here