AINA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuku wa kienyeji wapo aina nyingi.Hawa hutambulika kutokana na maumbile yao,sura,tabia na asili wanapotoka.
kuku bora wa kienyeji ni yule anayestahimili magonjwa,hali ya hewa ya mahali husika na mwenye uwezo wa kutaga mayai makubwa na wengi.pia yule mwenye kimo na mwili unaoweza kuwa mkubwa.
MIFANO YA KUKU BORA WA KIENYEJI NI KAMA IFUATAYO;
KUCHI;wana miili mikubwa,miguu mirefu na upanga wenye umbile la ua rozi.wanapatikana zaidi mazingira ya pwani
TEWE;waa miguu mifupi na miili midogo
BUKINI;Wana miili ya wastani lakini hawana manyoya marefu ya mikiani.wanapatikana zaidi ukanda wa pwani
NJANJAME;Wana manyoya yaliyokunamana,maumble mbalimbali na wanapatikana maeneo mengi ya nchi yetu.
KISHNGO;Hawa ni kuku wasio na manyoya shingoni na ndio asili ya jina lake.wana miguu mirefu na miili ya wastani.
baada ya kufahamu aina za kuku wa kienyeji napenda kuku onyesha magonjwa,dalili tiba na kinga kwa kuku
MDONDO(NEW CASTLE)
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi.unaathiri mifumo ya fahamu,chakula na upumuaji
DALILI
-kuku wengi kuugua kwa wakati mmoja hadi kufikia asilimia 100
-kuharisha kinyesi cha kijani na wakati mwingine chenye mchanganyiko wa damu
-kukohoa na kupumua kwa shida
-kujaa maji kwenye macho na kooni
-kutaga mayai yenye ganda laini na wakati mwingine halipo kabsa
-kuzubaa na kuacha kula
TIBA
Hakuna dawa ya tiba ila kuku wapewe dawa za viuavijisumu(antibiotics)
-zuia watu wageni kuingia ovyo kwenye mabanda hasa wanaotoka maeneo ya ugonjwa.
-zuia uingiaji wa kuku wageni wasio chanjwa
-kuku wapewe chanjo tangu vifaranga wa umri wa siku3,baada ya wiki 3-4 na baada kila baada ya miezi 3
NDUI YA KUKU(FOWL POX)
NI ugonjwa wa kuku unaosababishwa na virusi pia.
DALILI
-UPele kwenye ngozi ya kichwa,shingo na maeneo ya kutolea haja
-vipele mdomon na kohoni vinavyo sababisha kuku kushindwa kula
-kupumua kwa shida
TIBA
Pia hawana tiba ila kuku wapewe vitamin A na dawa za vijiua sumu (antibiotics) kama vile 'oxytetracycle 20% kuzuia magonjwa nyemelezi
kuku wapewe chanjo mara mbili umri wa wiki 4 na mwezi 1-2
kwa leo na omba tuishie hapo tutaonana kwenye makala nyingine panapo majaliwa
usisite kuandika maoni,maswali
Post a Comment