UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA


Kuku wa nyama/ broiler kwa lugha ya kingereza ni kuku ambao wanazalishwa kwa wingi sana hapa nchini tanzania, hiyo ni kwa sababu kuku hao wamekua na soko kubwa sana hapa nchini.
hivi nitaelezea angalau wewe mfugaji au mtu unae taka kufuga kuku hao upate mwanga.

  nitaanza na jinsi ya kutunza kifaranga kilicho fika kwa mara ya kwanza kwa sababu nilisha elezea hapo awali jinsi banda la kuku linavo takiwa kua.

 JINSI YA KUMTUNZA KIFARANGA ALIE FIKA KWA SIKU YA KWANZA
  
  Kifaranga kidogo kinatakiwa care sana ili kiweze kukua na kikiwa kina afya bora mpaka kufikia siku ya kuuza.
siku ya kwanza kifaranga kikisha fika kwenye banda kinatakiwa kupewa glucose kwa masaa nane 8 mfurulizo pamoja na vitamin, glucose inapewa kwa kuwanyunyuzia pamoja na kuwawekea kwenye maji na vitamin inapewa  kwa masaa 48/siku 2.
 

CHANJO/ VACCINATION
  
 NEWCASTLE, kifaranga anapo fika umri wa siku 5-7  kifaranga anatakiwa apewe chanjo hiyo ya newcastle.
baada ya hapo anapewa anti stress kwa sku 2 mfululizo

 GUMBORO, kifaranga anapo fika siku ya 14 anatakiwa apewe chanjo ya gumboro na baada ya baada ya apo apewe antstress kwa siku 2

unatakiwa uwanyime maji masaa 2 kabla ya ya kuwapa chanjo
nautakiwi kuacha naji yenye chanjo zaidi ya masaa 2

  KUWALISHA
1-7 kifaranga anatakiwa apewe bloiler stater mash.
8-14 unatakiwa uwalishe broiler grower mash
15 nakuendelea hadi siku ya kuwauza unatakiwa uwalishe bloiler finisher mash

na kunanjia nyingine ambayo unaweza kutumia 
1-14 unawapa bloiler stater mash
15 nakuendelea ukawapa bloiler finisher kutokana na uchumi wako


natumaini umesoma na kuelewa vizurio juu ya ufugaji wa bloiler  hivo ukifata hivo utaona matokeo mazuri kabsa..,
lakini pia usisite kuwasiliana na mimi pale utapo kua unaitaji ushauri au elimu zaidi..
asantee

  

No comments