KILIMO BORA CHA MBAAZI (PIGEON PEAS)



UTANGULIZI
Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri. Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini.Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 6 hadi 8 kwa hekta

MAHITAJI MUHIMU YA MBAAZI.
Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao hili.
Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.
Mbaazi hukua vizuri katika maeneo yenye wastani wa mua wa mm 400-1000 kwa mwaka,katika maeneo yenye mvua zaidi ya mm 1000 kwa waka hustawi ila ni rahisi kupta ugonjwa wa mnyauko.
Mbaazi hustawi vizuri katika hali ya joto ya nyuzi 18-30 C. Pia kama hali ya udongo na unyevu ni nzuri zinaweza kukua vizuri katika hata katika 35 C.

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI
Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.
Hustawi vizuri katika udongo wenye pH 5-7, Pia pH 4.5 - 8 zinaweza kulimwa

AINA KUU ZA MIMEA YA MBAAZI
*Kuna aina kuu tatu za mimea ya mbaazi*
Mbaazi za muda mrefu: Hii ni mbaazi ambazo zinawezwa kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake na kuruhusu Machipukizi yake kukua na kuvunwa tena msimu unaofuata na zoezi hili hufanyika ziadi ya msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa
Mbaazi za Muda wa kati; Hizi hulimwa kwa msimu mmoja ila huchukua mda wa kati katika kukomaa kwake.huchukua siku 140 hadi 180
Mbaazi za muda Mfupi:Hizi hulimwa kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung'olewa na kupandwa mbegu mpya msimu unaofuata.mbegu hizi huchukua siku 120 hadi 140.

MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kadri utakavyoweza kulima kulinga na aina ya kilimo unachotumia, hakikisha umeondoa magugu shambani na uchafu mwingine ambao unaweza kuinyima mimea ya mibaazi kukua vizuri.

UPANDAJI...
Mbaazi za Muda Mirefu; Panda kwa mistari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 150 kwa 100. (Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika mstari)
Mbaazi za Muda wa Kati; Mbaazi.Panda kwa mstari nafasi ya sentimeta 100 kwa 60
Mbaazi za Muda Mifupi;Panda kwa mstari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwa sentimeta 60

*ANGALIZO:*
Maaneo ya Pwani ambayo yanarutuba kwa wingi na joto la kutosha mimea inakuwa kwa kasi na ili upate mavuno bora lazima uhakikishe mimea yako unaipa nafasi ya kutosha,Hivyo uwe makini na nafasi za mimea yako uanapopanda shambani.

MATUMIZI YA MBOLEA.
Mara nyingi zao la mbaazi halihitaji matumizi ya mbolea na samadi. Ijapokuwa Hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.
PALIZI

Mimea ya mibaazi huitaji kupaliliwa mapema ili kufanya ikue katika hali ya afya bora na kusaidia kuongeza mavuno yako.

WADUDU WANAOSHAMBULIA MIBAAZI NA MBAAZI
Mbaazi ni mojawapo ya mazao ambayo hayashambuliwi sana na wadudu japokuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi. *Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama ATTAKAN-C,Karate au dawa nyingine za wadudu.*

MAGONJWA YA MBAAZI
Ugonjwa mkuu unaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa fusaria ( fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi nyeusi,ugoro au kahawia.ugonjwa huu huzuia mfumo wa usafirishaji wa mmea.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani kila baada ya msimu kuisha.usipande kila msimu mbaazi tuu.Kila msimu badilisha zao.

UVUNAJI WA MBAAZI
Mbaazi zikishakomaa na kuanza kukauka zivunwe mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kisha Mbaazi zitenganishwe kwa mikono au kwa kupigwa hayo matawi taratibu baada ya kukaushwa sana.


BOFYA VIDEO CHINI KUJIFUNZA MAMBO MENGI ZAIDI

No comments