Taabu Shambani: Wakulima wa Kahawa ya Afrika Wanapoteza Mabilioni kwa Unyonyaji
● Mkulima wa Afrika anazalisha baadhi ya kahawa yenye ubora wa juu zaidi, lakini hupokea bei hafifu zaidi kuliko wazalishaji wote, ulimwenguni.
● Wakulima wa kahawa ya Afrika wanapoteza dola bilioni 1.47 kila mwaka kutokana na unyonyaji wa bei za mazao yao.
● Kutokana na mazingira ya biashara yasiyo na usawa, wakulima wa kahawa wa Ethiopia na Uganda wanakadiriwa kupoteza dola za kimarekani milioni 713.1 na dola za kimarekani milioni 229.7 kwa mfuato huo, katika mwaka mmoja pekee.
● Suluhisho muafaka pekee ni utengenezaji wa Makubaliano ya Kimataifa ya Kahawa, yenye msingi wa ugavi, ambayo yataweka ugavi wa mauzo na hivyo kusaidia kuziendesha bei.
NAIROBI, 27 Julai 2020 – Mamilioni ya familia za wakulima kutoka kote barani Afrika zinakumbana na uzorotaji wa kiuchumi kadri bei za kahawa wanazopatiwa zikiendelea kuzorota kuelekea chini, mara nyingi chini ya gharama za uzalishaji. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Taabu Shambani: Wakulima wa Kahawa ya Afrika Wanapoteza Mabilioni kwa Unyonyaji ambayo imetolewa hivi punde na Selina Wamucii. Ripoti hii inatoa mtazamo wa msingi na wa hivi karibuni unaohusu namna wakulima wa kahawa ya Afrika wanavyonyonywa hadi kifo, katika tasnia inayotengeneza mabilioni ya dola kila mwaka.
Kwa mujibu wa ripoti hii, sehemu ya wakulima wa Afrika katika thamani ya kahawa huanzia asilimia 8.7 hadi 12.6, huku sehemu hii ikiwa ndogo kulinganisha na iliyopo kwa wauzaji wakubwa wa kahawa ya Afrika, Ethiopia na Uganda, ambayo iko katika asilimia 12.6 hadi 10.0 vivyo hivyo. Sehemu ya wakulima kwenye mlolongo wa thamani ya kahawa iliyokokwa ni kubwa nje ya Afrika, huku wakulima wa kahawa ya India wakipata asilimia 15.7 nchini India na 14.9 nchini Brazili.
Kutokana na mazingira yasiyo na usawa, mapato yanayopotezwa kila mwaka kutoka kwa wakulima wa Ethiopia ni dola za kimarekani milioni 713.1 na dola za kimarekani milioni 229.7 kwa wakulima wa Uganda; hii inakadiriwa kwamba wakulima wa kahawa ya Afrika wanapoteza dola za kimarekani bilioni 1.47 kila mwaka kutoka kwenye unyonyaji wa bei za mazao yao.
Viasi hivi ni muhimu kwa wazalishaji wa Afrika kutoka nchi kadha wa kadha ambazo kahawa ni zao lake kuu linalosafirishwa nje ya nchi.
Kwa Wanjiru Kariuki, mkulima wa kahawa mwenye miaka 68 kutoka Othaya, mathalani kilomita 120 kaskazini mwa Nairobi, anatafakari namna gani mkulima wa kahawa anaweza kuwa maskini kupindukia wakati faida za walanguzi wa kimataifa wa kahawa zikizidi kuongezeka mwaka baada ya mwaka.
"Tazama mkanda huu unaobana – unashikilia tumbo langu ndani na unanisaidia kuepuka maumivu ya njaa”, alisema Wanjiru, akinyoosha mkono kuelekea kiuno chake.
"Mimi ni fukara, nina njaa, na sina viatu. Wale wanaonufaika kutoka kwenye kazi zangu ngumu hawawezi hata kufunga mkanda kama hivi kwani matumbo yao ni makubwa kuliko kiboko, yote kutokana na kahawa yangu” aliongeza bibi wa wajukuu wanne.
Kwa mujibu wa John Oroko, Mkurugenzi Mtendaji wa Selina Wamucii, hali hii inamchanganya sana mkulima wa Afrika, ambaye anazalisha kahawa yenye ubora safi, lakini anapokea bei hafifu kuliko wakulima wote, ulimwenguni. Wakulima hawa wa kahawa wanahatarishwa kwa kweli.
“Suluhisho muafaka pekee ni utengenezaji wa Makubaliano ya Kimataifa ya Kahawa, yenye msingi wa ugavi, ambayo yataweka ugavi wa uuzaji wa nje, na kusaidia kuendesha bei, hivyo kuwawezesha wakulima kuishi kutokana na mavuno ya kazi zao ngumu,” anasema Bw. Oroko.
“Kama Afrika inataka kukomesha unyonyaji unaowamaliza wakulima wake wa kahawa, kanuni za kimataifa za biashara ya kahawa zitabidi kubadilishwa kupitia mfumo wa siasa unaohusu mkulima. Na kama hili haliwezi kufanyika ndani ya mipaka ya Shirika la Biashara Duniani (WTO), basi Waafrika afadhali waitazamie OPEC kuhamasisha na kutekeleza Makubaliano ya Kahawa ya Muungano wa Afrika, ambayo hayatanenepesha watu wachache huku ikinyonya maisha ya wakulima. Kitu kingine chochote tofauti na hichi, ni ishara tu ya kutafuta kusogeza muda.” alimalizia Bw. Oroko.
Taabu Shambani: Ripoti ya ‘Wakulima wa Kahawa ya Afrika wanapoteza Mabilioni kwa Unyonyaji’ inapatikana
Kuhusu Selina Wamucii
Selina Wamucii ni jukwaa la chakula na mazao ya kilimo kutoka mashirika ya kilimo ya Afrika, makundi ya wakulima, wasindikaji wa mazao ya kilimo na asasi nyingine ambazo hufanya kazi moja kwa moja na familia za wakulima kutoka nchi 54 za Afrika.
Selina inawaweka wazalishaji wote wa Afrika (ambao asilimia 80 ni familia za wakulima) na mazao yao kwenye jukwaa moja ambalo wanunuzi kutoka kokote duniani wanaweza kupata kwa urahisi na kununua mazao kutoka Afrika.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:
Timu ya Selina Wamucii ya Mawasiliano na Taarifa
Simu: +44 808 164 1995
Barua pepe: press@selinawamucii.com
Wavuti: https://www.selinawamucii.com/press/
Post a Comment