kILIMO CHA PARACHICHI "FURSA" MTI MMOJA UNAKUPA KATI YA 300,000- 700,000


 Sijambo la ajabu kuona baadhi ya mazao yamekua yakiwaingizia wakulima pesa nyingi, hutegemea na uongezeko wa uhitaji. mfano tumekua tukisia kuhusu kilimo cha tikiti, vitunguu, tangawizi kuwatajilisha wakulma wengi hii si ajabu. Kama wewe ni mfatiliaji umeshakia kuhusiana na kilimo cha parachichi kinavyo shika kasi kwa sasa

tumeona watu wengi wakizungumzia jinsi ambavyo maparachichi yamekua yakiitajika kwa sasa. mimi pia nilijaribu kupitia sorces mbalimbali ili niweze kufahamu ukweli kuhusiana na hili. na niukweli usiopingika kwamba zao hili limekua likitajika kwa kiasi kikubwa. na vyanzo mbalimbali vinasema kwamba uhitaji umeongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa uelewa na uhamasishaji wafaida za parachichi katika afya, ambapo kwa imeelezwa kwamba kutokana na uelewa na hali ya watu kupenda afya zao kwa sasa wamekua wakifata ushauri wanamna gani wanaweza kufanya afya yao kua bora kwa kula vyakula vya asiri. Na tunapo zungumzia parachichi ni moja kati ya tunda lenye virutuisho vya kipekee kama OMEGA Hivyo watu wamekua na msukumo mkubwa kutumia parachichi na imepelekea soko la dunia kupanda kwa kiasi kikubwa.

 Sasa hii ni fursa kwa wakulima nchini kwani tumekua tukiona kwenye vyombo vya habari jinsi nchi mbalimbali kama vile Israel zikionesha uhitaji wa zao hili, hata hapa africa south africa na kenya ni moja kati ya nchi ambazo zinazarisha parachich kwa wingi sana na wamekua wakipata pesa nyingi kuptia zao hilo. Lakini hata juzi juzi tumesikia jinsi Uganda inavyo onyesha nia ya kuongeza nguvu katika uzarishaji wa zao hili. Na hata hapa kwetu tanzania licha ya kua bado watu wengi hawajaichangamkia fursa hii, tumekua tukiona shuhuda mbalimbali kwani ukianngalia mikoa ya njombe, mbeya na iringa ambapo zao hili linasitawi vizuri sana. kuna baadhi ya wakulima wekilima zaidi ya heka 90, na wengine wanaingiza faida hadi bilioni kwa mwaka.

TAZAMA VIDEO KUFAHAMU ZAIDI


 

 

Post a Comment

0 Comments