MKULIMA:Nimelima "VITUNGUU EKARI 1 NIKAPATA GUNIA 70" Nategemea million 20




Kama wewe ni mfatiliaji wa mambo ya kilimo, bila shaka utakua unafahamu kwa sasa
zao la vitunguu limepanda bei sokoni. kwani katika maeneo mengi kilo 1 ilikua inauzwa
shilling elfu 1 na sasa sehemu nyingi inauzwa hadi shillingi elfu 2.

hii ni kutokana na sababu kwamba maeneo mengi ni msimu wa mvua kubwa,
na kama tunavyo fahamu nikwamba vitunguu havifanyi vizuri katika msimu wa mvua kubwa.
hivyo imepelekea bei ya vitunguu kupanda bei na gunia linaweza kufika hadi shiling laki 2.

leo nilipata fursa ya kuzungumza kwa njia sms na moja kati ya wadau wetu hapa rubaba tv,
ambae pia kwa muda amekua akilima vitunguu. na yeye kwa msimu huu alilima ekari moja ya
vitunguu ambayo amefanikiwa kupata zaidi ya gunia 70 kwa makadirio. ambapo yeye anasema kwa
hali iliyopo sokoni kwa sasa anategemea kupata zaidi ya milioni 20.

kuna baadhi ya vitu ambavyo alivizungumza na nikaona nivyema niweze kushare na wewe pia kama
ni mkulima wa vitunguu au unapenda kufanya kilimo hiki uweze kujifunza kutoka kwake.

1. Mwanzoni alikua akilima eneo kubwa sana, ambalo lilikua likitesa na kutumia gharama nyingi
na mwisho wa siku alipata hasara, baada ya kugundua aliamua kuacha na kulima ekari moja tuu.
na kwa mujibu wake haikumpa presha sana na aliweza kumudu gharama.

2. Mwanzoni alikua akituma pesa bila kufika shambani, na mara kadhaa amekua akitapeliwa au kukuta
pesa aliyotuma haiendani na kazi iliyofanywa. msimu huu alikua mfatliaji na anashangaa mambo yote
yalienda kama yalivyo pangwa.

3. mwishoni alisema anashukuru kwa sababu ameweza kuvuna msimu mzuri, mwanzoni alikua anapata magunia
machache na kuishia kuuza kwa bei ndogo, sababu wengi walikua wamelima.

TAZAMA VIDEO KAMILI



No comments