Nilivyokua chuo "NILIWEKEZA HIVI Nilipata faida kupitia kilimo



Siku za karibuni nilikua nikibadilishana mawazo na marafiki zangu,
ambao baadhi nilisoma nao chuo lakini wengine walikua wamenitangulia.
 na wao wanaendesha maisha yao kupitia kilimo na ufugaji, wengine wakilima/ kufuga,
moja kwa moja wengine wakifanya shughuri tofauti lakini katika sekta kilimo na ufugaji.

uzuri ni kwamba wengi wao walikua wameanza harakati hizo tangia wako vyuoni na wengi
wao ndio zimekua shughuri zao mpaka sasa, na nikaona nivyema katika kipindi cha leo
nizungumzie kidogo jinsi gani hata wewe kijana amabae upo chuo au upo nyumbani, unaweza
kujifunza mbinu hizi ambazo wenzetu wamekua wakizitumia kuweza kujitengenezea ajira kupitia
kilimo na ufugaji.

1. mmoja yeye alikua akitumia kipindi cha likizo kuweza kulima mazao ya msimu kijijini kwao.
na anasema alikua akilima vitunguu na hadi sasa ndio kitu ambacho anakifanya kwaajili ya kumpa kipato
cha kila siku.

2. mwingine alikua akinunua mazao kipindi cha mavuno mengi kwa bei nafuu na amekua akiuza wakati bei
imekua juu, ni imekua ikimpatia kipato kikubwa na nimoja kati ya shughuri ambayo hua anaifanya mara nyingi.

3. Mwingine yeye aliamua kuanzisha genge sokoni na wakati wa asubuhi amekua akiamka kufata bidhaa mbalimbali
na wakati wa masomo amekua akimuajili mtu kuweza kumuuzia.

4. wengine waliamua kuchanga pesa na kufanya kilimo cha pamoja na iliwasaidia kuweza kupata pesa na hata kuendeleza
shughuri hyo baada ya masomo.

5. lakini wengine nimekua nikiwashuhudia wakiuza bidhaa za kilimo mbalimbali kwa kuzitoa sehemu ambapo zinapatikana
kwa bei nafuu na kuuza kwa faida.


TAZAMA VIDEO KAMILI



Post a Comment

0 Comments