🐖 MAMBO YA MSINGI KABLA YA KUANZA UFUGAJI WA NGURUWE

0


Wafugaji wengi huingia bila maandalizi, wakidhani faida inapatikana mara moja – kumbe msingi ni mpangilio na maarifa ya awali. Haya ndiyo mambo ya lazima kabla hujaanza:

1️⃣ Soko

Usiingie bila kujua unamfugia nani.

  • Tafuta wateja wa moja kwa moja kama butcheries, hoteli, minada au viwanda vya nyama.

  • Kumbuka: madalali mara nyingi hununua bei ndogo, wakichukua faida yako.

2️⃣ Mbegu Bora

Nguruwe bora ndio msingi wa mafanikio.

  • Chagua mbegu zinazojulikana kukua haraka kama Landrace, Large White, Duroc au mchanganyiko wa kitaalamu.

  • Sifa za kuangalia: mwili mrefu, mgongo ulionyooka, miguu imara, macho makali, ngozi yenye afya.

  • Hakikisha mbegu hizo hazijatokana na kizazi kimoja ili kuepuka matatizo ya vinasaba.

3️⃣ Lishe

Lishe ndiyo injini ya ukuaji.

  • Piglets (wiki ya 3–10): wanahitaji chakula chenye protini ya juu (16–18%) na hupunguza haraka.

  • Growers (miezi 3–5): wanahitaji 14–16% protini na virutubisho vya madini.

  • Kwa ukuaji wa kawaida, nguruwe anaweza kula kati ya 2.5 – 3.5kg za chakula kwa siku kulingana na umri na uzito wake.

  • Kwa lishe sahihi, nguruwe anaweza kuongeza uzito kati ya 700–800g kwa siku.
    👉 Hii ndiyo maana ya kutumia feed bora zenye usawa, mfano zile za Koudijs, ambazo zimetengenezwa mahsusi kwa piglets na growers.

4️⃣ Makazi

Banda bora = nguruwe wenye afya.

  • Nguruwe mmoja anahitaji angalau 1.2 – 1.5 m².

  • Banda liwe safi, lisilo na unyevunyevu, na lenye hewa ya kutosha.

  • Weka maji safi ya kunywa muda wote – nguruwe wa kilo 60+ hutumia wastani wa lita 6–8 za maji kwa siku.

5️⃣ Mpangilio wa Uendeshaji

  • Jiandae na ratiba ya chanjo na kinga magonjwa.

  • Panga ufuatiliaji wa uzito na ukuaji kila wiki.

  • Usisahau kuweka akiba ya chakula cha mwezi mzima kabla hujaanza, ili usikwame katikati.

✅ Ukiwa umezingatia haya mambo, unakuwa umejenga msingi thabiti wa biashara ya nguruwe.

👉 Kwa mwongozo wa kitaalamu na mafunzo ya kina, unaweza kujiunga na jumuiya yetu ya Tanzania na Kilimo kwa kutuma neno NIUNGE WhatsApp hapa:
🔗 https://wa.me/255764148221

TAZAMA VIDEO YA UFUGAJI WA NGURUWE KIBIASHARA



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

write your comment here

write your comment here

Post a Comment (0)

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top