KILIMO BORA CHA MBAAZI
Mbaazi ni moja kati ya mazao yanayo limwa kwa wingi nchini Tanzania
Hali ya
hewa inafaa kwa kilimo kwa kilimo mbaazi
ni nyuzi joto 18 hadi 38sentigredi.mbaazi huwa hazivumialii barafu .Mbaazi
hustawi kwenye mvua kwa mwaka kiasi cha milimita 600 hadi 1000 inagawa aina za
muda mfupi hustawi kwenye kiwango kidogo cha mvua milimita 250.hazistawi zaidi
kwenye usawa wa bahari
AINA ZA
MBAAZI
Kuna makundi
makuu matatu ya zao la mbaazi
MBAAZI ZA MUDA MREFU
Huchukua
miezi sita mpaka saba shambani mpaka wakati wa kuvuna.
Zina matawi
machache na ni ndefu hvyo hufaa sana kwa kilimo mseto.haini zinaweza kuvunwa
zaidi ya msimu mmoja lakini mazao yanayopatikana baada ya msimu wa kwanza huwa
madogo hivyo inashauriwa aina zipandwe upya kila mwaka
USTWAI;Aina
hizi hustawi vizuri katika ukanda wa juu na kati wenye mvua za kutosha .
MBAAZI ZA MUDA WA KATI
SIFA ZAKE
Hukomaa
ndani ya muda wa miezi minne na nusu mpaka miezi sita baada ya kupandwa.zina
matawi mengi na ni fup kulingana na mbaazi za muda mrefu.hazikomai zote kwa
wakati mmoja humlazimu mzalishaji kuvuna zaidi ya mara moja ingawa mazao ya
kwanza ni mengi kuliko mazao yanayofata.zinapendwa na kina mama kwa sababu ya
mboga kwa jili ya mboga au enderefu kwa sababu huchanua tena mara zikipata maji
USTAWI;Aina
hii ya mbaazi hulimwa katika ukanda wa kati mita 800 hadi 1100 usawa wa bahari
zenye mvua za wastani
MBAAZI ZA MUDA MFUPI
Kundi hili
linawakilisha aina bora za mbaazi za muda mfupi yaani miezi 3 hadi 3 na nusu.
SIFA ZAKE
Aina hii ni
fupi ni mita moja hadi moja na nusu yenye mauwa mekundu inapoanza kuchanua
hulimwa katika ukanda wa kati na wa chini katika uhaba wa mvua kama vile maeneo
ya pwani
Aina hii
hazichanganywi na mahindi ,inahatari ya kushambuliwa sana na wadudu hasa ukanda
wa kati na wa juu sababu huchanua wakati wa mvua
Tofauti na
aina zote za mbaazi aina hii haiasiliwi nan a urefu au ufupi wa siku hivyo
itachanua wakati wowote mara baada tu ya kupanda
Haina hii ya
mbaazi haina ukinzani wa ugonjwa wa kunyauka
MATUMIZI YA MBAAZI
Chakula kwa
binadamu
Kilimo cha
mseto,mbaazi za muda wa kati na muda mrefu zinaweza kulimwa mseto na mzao
mengine ya jamii ya nafaka mfano mahindi , mtama ,uwere
FAIDA ZA KULIMA MBAAZI NA MAZAO
MENGINE
1 Matumizi
bora ya ardhi hasa kwa kuwa mbaazi huongeza ufyonzaji wa hewa ya naitrogen
shambani
2 Mzalishaji
atapata mazao mawili au zaidi katika shamba mojana msimu mmoja
3 Kipato cha
mzalishaji kitaongezeka kutokana na mazao mengine
4 Pia mafuno
ya mazao ya nafaka kama mahindi hayapungui kwa kiasi kikubwa kutokana na
mchango huo wa mazao
UTAYARISHAJI WA SHAMBA
1 N’goa
visiki pamoja na mabaki yote ya mimea kabla ya uzalishaji
2 Lainisha
udongo kwa kupiga halo mbaazi zinavyoota huwa dhaifu sana na kama shamba
halikuandaliwa vizuri magugu huota mapema kabla ya mbegu za mbaazi
3 Tayarisha
matuta au makinga maji kama shamba lipo kwenye mteremko .
KUANDAA MBEGU
Mbegu bora
iliyochaguliwa vizuri na kuhakikiwa kiwango cha uwotaji iandaliwe
Mbegu ziwekwe dawa za kuzuia kuvu kabla ya
kupanda ili kuzuia magonjwa yatokanayo na mbegu na udongo
MBEGU BORA
Mbegu za
mbaazi zimegawanywa kwenye makundi makuu matatu
1 mbegu ya
mda mfupi
2 mbegu ya
mda wa kati
3 mbegu ya
mda mrefu
UOTESHAJI
Nafasi
kutoka mstari hadi mstari hutegemea zao kuu linalopandwa .kilimo mseto na
mahindi hutegemeana pia na aina za mbegu sentimita 90 mpaka 120 sentimita
unashauliwa kutoka mstari hadi msatri 50 sm kutoka shimo hadi shimo acha mimea
miwili kwa shimo
Panda
mahindi yanayo komaa mapema ili yavunwe mapema na kutoa nafasi kwa mbaazi ili
kuchanua na kutanuka
Tumia kilo 4
hadi 5 kwa hekari kutegemeana na ukubwa wa punje
UPANDAJI
Mbaazi za
mda mrefu panda kwa mistari kwa umbali wa sm150 kwa sm100
Mbaazi za
muda wa kati panda kwa mstari wa sm100 kwa 60sentimita
Mbaazi panda
kwa umbali wa nafasi sm90kwa 60sentimita
MBOLEA
Mbaazi
hustawi vizuri kwenye shamba lenye mbolea ya kutosha.Hivyo inapendekezwa kwamba
kila mzalishaji aweke mbolea ya samadi ili kuhifadhi arhdi dhidi ya upotevu
mkubwa wa mbolea
Jamii ya
mikunde hujitengenezea aina ya mbolea ya naitrogen . hata hivyo tafiti
zinaonesha kwamba matumizi ya mbolea za kupandia kama mabolea ya minjigu
,TSP,OAP,kutaimarisha mizizi na mshina na hivi kuongeza uzalishaji
PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA
Ni muhimu
kuoalilia mapema kuondoa magugu ambayo hushindana na mimea .palizi ifanyike
mara mbili kwa wakati.palizi tatu inategemea wingi wa majani na unyevu au mvua
. mishe ikiwa mingi kwenye shina husabsbisha mazao kidogo kutokana na mimea
kushindania mwanga na virutubisho. Palizi inaweza kufanyika kwa jembe la mkono
au trector kulingana na nafasi iliyotumika katika kupanda . palizi mbili za
mwanzo kati ya siku 60 za mwanzo ni muhimu kbla ya mbaazi hazijawa na kivuli
cha magugu kumea lakini pia kiuwa gugu kinaweza kutumika kabla ya mbaazi kuota
.baada ya mbaazi kuota dhidi ya magugu ya majani mapana ichanganywe
Fluazifopbutyl kudhibiti magugu jamii ya nyasi,kiuwa gugu kitumike wakati
mbaazi zimekua kufikia sentimita 25 hadi 30 .Nimuhimu kupunguzia miche na
kubakiza miwili au kutegemeana na nafasi iliyo tumika
UVUNAJI WA MBAAZI
Mbaazi
zikisha komaa na kuanza kukauka zivunwe mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi
na kukausha zaidi kisha mbaazi zitenganishe kwa mikono au kwa kupigwa hayo mati
taratibu baada ya kukaushwa sana
Post a Comment