Kutoka Kuku 200 Hadi Kampuni Kubwa Inayozalisha Trey Zaidi ya 100 za Mayai kwa Siku

2

Wakati wengi wakidhani kuwa mafanikio makubwa katika ufugaji yanahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia, KOWNAS INVESTMENT LIMITED  imevunja dhana hiyo. Kampuni hii ilianza safari yake ya ufugaji kwa kuku wa mayai 200 tu Mwaka 2019, lakini leo hii ni mojawapo ya miradi mikubwa ya mfano nchini Tanzania, inayozalisha zaidi ya tray 100 za mayai kwa siku.

Safari yao ya mafanikio si ya kawaida. Kwa miaka kadhaa sasa, Kampuni hii imekuwa ikijikita katika ufugaji wa kibiashara kwa nidhamu na kutumia mbinu bora. Moja ya siri kubwa ya mafanikio yao ni matumizi ya bidhaa bora za lishe ya mifugo kutoka Koudijs, zinazosaidia kuku wao kuwa na afya njema, uzalishaji mkubwa na gharama ndogo za matibabu.

Katika ziara ya Rubaba TV kwenye shamba hili, tulishuhudia namna ambavyo  wamewekeza kwenye usafi wa mazingira, usimamizi wa chakula, na teknolojia rahisi zinazorahisisha kazi. Ni dhahiri kuwa mafanikio yao yanatokana na maamuzi sahihi, elimu ya kutosha kuhusu ufugaji, na kutumia bidhaa zenye ubora wa kimataifa.

Kupitia video hii utakayoweza kuitazama kwenye Rubaba TV, utajifunza mengi kuhusu:

  • Jinsi ya kuanzisha ufugaji wa kuku wa mayai kwa mtaji mdogo

  • Namna ya kuongeza uzalishaji kwa kutumia lishe sahihi

  • Faida za kutumia bidhaa za Koudijs kwenye shamba lako

Usikose kutazama video hii ya kipekee na kujifunza kutoka kwa waliopitia changamoto hadi mafanikio.
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 Shamba: 0758 161 109
📞 Koudijs Kanda ya Ziwa: 0765 321 406




Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

write your comment here

write your comment here

Post a Comment

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top